Skip links

VicobaStore

VicobaStore

*VicobaStore*

Mfumo huu ni mahususi kwa ajili ya hifadhi taarifa za fedha za vikundi vya kijamii kama vile vicoba, unaweza hifadhi taarifa za mikopo, jamii, hisa, mapato na matumizi ya kikundi, pia wakopeshaji binafsi wanaweza tumia.

Kwa kutumia mfumo huu kunakuwa na uwazi wa taarifa za kikundi kwani kila mwanachama anaweza kuona taarifa zote za fedha,

Hivyo mhazini anakuwa amepunguziwa kazi ya kuandaa taarifa za fedha kila wakati.

*Miamala*
-Kuweka fedha kwenye akiba, hisa na jamii kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake

-Kutoa fedha kwenye akiba, hisa na jamii kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake

-Mikopo (kukopesha, kurejesha na kufuta mkopo kwa kila mwanachama kwenye akaunti yake)

-Kuhifadhi mapato na matumizi ya kikundi

-Kuhamisha fedha kutoka taslimu kwenda benk/kutoka benki kwenda taslimu

-Marejesho ya mkopo ni automatically, ila kuna option ya kulipa manually

*Ripoti*
-Mikopo yote ya kikundi na kuonesha salio la msingi, malimbikizo na riba ghafi

-Orodha ya masalio ya akiba, hisa na jamii

-Taarifa ya mapato na matumizi

-Salio la fedha taslimu na kiasi kilichopo benki

– Orodha ya michango yote kama rejesho,savings,hisa,akiba na jamii kwa ajili ya kupost kila mwisho wa mwezi, hivyo mhasibu hana haja ya kuandala orodha nyingine for posting

-Riba ghafi(accrued interest) kwenye akiba zako ambayo inakuwa automatically calculated on daily basis, hii ndio inayotumika kwenye dividend payment.

-Idadi ya wanachama wote

*NB* mwanchama ambaye si mhasibu atakuwa anauwezo wa kuona taarifa zake zote, kwa maana ya
1.Salio la akiba
2.Salio la hisa
3.Salio la jamii
4.Taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi
5. Idadi ya wanachama wote wa kikundi
6.Jumla ya bank/cash balance.
7. taarifa fupi (Min statement) ya akiba,hisa,jamii na mkopo mpaka miamala 15 ya karibuni
8. Taarifa ndefu (statement)
9. Mchanganuo wa rejesho la mkopo ya akiba,hisa,jamii na mkopo

*NB* Mwanchama anaweza omba mkopo kupitia app na email itaenda moja kwa moja kwa mhasibu,katibu, mwenyekiti na nakala kwa mwombaji, na baada ya kupewa mkopo, taarifa itatuma kwa mwombaji wa mkopo